January 17, 2014



Kocha Mkuu mpya wa Yanga, Hans van Der Pluijm ameanza kazi rasmi kukinoa kikosi cha timu hiyo asubuhi na jioni jana.
Van Der Pluijm raia wa Uholanzi, ameanza kwa kufanya mazungumzo na wachezaji hao na kuwataka wacheze soka la haraka na kuachia pasi haraka au kugusa tu.


Akizungumza kutoka Antalya, Uturuki, Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema van Der Pluilm aliwataka wachezaji wake kucheza mpira wa kuachia na kuchukua nafasi.

“Kwanza wamemfurahisha, hakutegemea kuona timu inacheza kwa kasi na kujituma,” alisema Kizuguto.

“Kocha aliishuhudia timu kwa mara ya kwanza wakati ikicheza mechi ya kirafiki. Amezungumza na wachezaji na kuwaeleza mambo kadhaa ikiwemo kusisitiza uchezaji wa kuachiana pasi badala ya kubaki na mpira kwa muda mrefu.

“Lakini amesisitiza kwamba anataka wacheze kwa kujiamini na kama upungufu wa mambo ni kidogo sana na marekebisho yatafanyika, lakini kocha amekifurahia kikosi,” alisema Kizuguto na kuongeza.

“Amewaambia wachezaji mambo mengi tu, lakini amesisitiza kuwa fiti, kazi na ubunifu kwa ajili ya kufanya vizuri.”  

Kwa mara ya kwanza, van Der Pluijm alifanya mazoezi ya taratibu na kikosi hicho asubuhi jana na jioni alitarajia kuendelea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic