Mabao mawili ya Daniel Sturridge, moja
na nahodha Steven Gerrard na moja la Luis Suarez yameisaidia Liverpool
kuwavuruga watani wao wa jadi Everton kwa mabao 4-0.
Katika mechi hiyo ya watani wa jadi wa
jiji la Liverpool, Everton walishindwa kuonyesha makali yao kabisa na kulala
kwa mabao hayo.
Eveton ndiyo ilionekana kuwa na kikosi
kigumu zaidi kufungwa katika Premiership, lakini ilishindwa kuonyesha ugumu huo
na kuruhusu mabao manne.
Bahati kwa Everton ingeweza kulala kwa
mabao matano, lakini Sturridge alikosa penalti kwa mkwaju aliopiga kupaa juu ya
lango la watani wao hao wa jadi.
MATOKEO MENGINE:
Swansea 2 Fulham 0
Crystal Palace 1 Hull City 0
Norwch 0 Newcastle 0
MATOKEO MENGINE:
Swansea 2 Fulham 0
Crystal Palace 1 Hull City 0
Norwch 0 Newcastle 0
0 COMMENTS:
Post a Comment