Arsenal imeponea chupuchupu baada ya
kutoka sare ya mabao 2-2 na Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu England uliomalizika
punde.
Katika mechi hiyo ambayo Arsenal
walionekana kuwa na mwendo wa taratibu sana, mabao yao yalifungwa na Olvier
Giroud na Santi Cazorla, wakati Southampton waliocheza vizuri zaidi yalifungwa
na Jose Miguel na Adam Lallana.
Kiungo Mathieu Flamini alilambwa kadi
nyekundu katika dakika ya 80 na kusababisha Arsenal ishambuliwe muda wote hadi
mpira unakwisha.
0 COMMENTS:
Post a Comment