Klabu za Simba na Yanga zimeukubali
uteuzi wa Juma Nkamia kuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo.
Nkamia ambaye aliwahi kuwa mtangazaji wa
Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kondoa Kusini
kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), alitangazwa kuchukua nafasi hiyo Jumapili
badala ya Amos Makalla ambaye amepelekwa kuwa Naibu Waziri Wizara ya Maji.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti,
viongozi wa Simba na Yanga wamesema Rais Jakaya Kikwete hakufanya makosa
kumteua Nkamia katika nafasi hiyo kwani anakidhi vigezo.
“Nimefurahi kuona rais amemteua Nkamia
na huenda akakumbuka alipotoka na atawaendeleza wanamichezo zaidi katika
kuhakikisha sekta ya habari inakua.
“Ni nafasi yake ya kuweza kuonyesha
uwezo kwani anafahamu vitu vingi vya michezo na kwa undani zaidi tofauti na
wengine waliokuwa wakipewa nafasi hivyo,” alisema Beno Njovu, Katibu Mkuu wa
Yanga.
Aidha, kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kamati ya Ufundi ya Simba, Danny Manembe, alisema Simba wana imani Nkamia
atasaidia soka na kuendeleza mbele tasnia ya habari kwa ujumla.
0 COMMENTS:
Post a Comment