Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic
amesema ana imani kubwa na safu yake ya ulinzi na anahamisha mashambulizi kwa
viungo.
Logarusic
amesema katika mashindano ya Mapinduzi amefurahia safu yake ya ulinzi
inavyocheza.
“Wanacheza vizuri, siwezi kusema
nimeridhika, lakini naweza kusema wanacheza vizuri.
“Ndiyo maana nilitaka kumsajili Ivo na
Musoti kwa ajili ya kuimarisha safu ya ulinzi.
“Ila sasa nitahamia kwa viungo kwa ajili
ya kuwaweka vizuri na baadaye washambuliaji.
“Bado kuna mambo sifurahii, lakini
najua, katika mafunzo lazima urudie tena na tena ili watu waelewe,” alisema
Logarusic ambaye msaidizi wake ni Selemani Matola.
0 COMMENTS:
Post a Comment