Winga nyota wa zamani wa Yanga, Edibily
Lunyamila amerejea katika hali nzuri na kuwashuruku wadau.
Lunyamila amesema anajisikia vizuri
tofauti na hali iliyomkuta hadi kulazimika kulazwa.
“Kweli nina nafuu kubwa, naona nimepona
ingawa ninahitaji muda kurudi katika hali yangu ya kawaida,” alisema Lunyamila.
“Natoa shukurani kwa wote walionijali,
walinipa faraja na walionyesha upendo wa juu kwa kweli, nashukuru sana,”
alisema Lunyamila.
Winga huyo alilazwa kwa zaidi ya wiki
moja kwenye Hospitali ya Mwananyamala kutokana na kusumbuliwa na magonjwa ya
moyo yaliyosababisha apumue kwa tabu hadi kuwekewa mashine ya kumsaidia
kupumua.
0 COMMENTS:
Post a Comment