Kipa Yaw Berko wa Simba amekalia kuti
kavu katika timu hiyo baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, Zdravko Logarusic,
kutaka amtumie Ivo Mapunda zaidi katika kikosi chake cha kwanza.
Ivo alipewa nafasi ya kukitumikia kikosi
hicho katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyomalizika hivi karibuni visiwani
Zanzibar na hatimaye kuibuka nafasi ya pili.
Kocha
wa makipa wa Simba, Idd Pazi, alisema kuwa awali walihitaji kumpumzisha Ivo
kufuatia kudaka mfululizo katika michuano hiyo, lakini kocha Loga amekataa na
kutaka kumtumia kipa huyo kwa kuwa kiwango alichokionyesha kwenye michuano ya
Mapinduzi ni kikubwa.
“Loga amekataa kumpumzisha Ivo kwa kuwa
alihitaji kukiona kikosi chake kilichocheza Mapinduzi ndicho kicheze mechi za
ligi kwani ameona ligi ni ngumu, hivyo anahitaji kumtumia ili aweze kuisaidia
timu na kama ulivyoona, tumeshinda.
“Nadhani kocha tayari ameshapata kikosi
ambacho ni kile kilichoshiriki Mapinduzi na iwapo kutakuwa na mabadiliko basi
yatakuwa machache,” alisema Pazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment