Uongozi wa Yanga umesema wala hauna
presha na majibu yatakayotolewa na Fifa kwa kuwa tayari wameshapata ruksa
kutoka Caf ya kumtumia mshambuliaji wao Emmanuel Okwi kwenye michuano ya Klabu
Bingwa Afrika dhidi ya Komorozine ya nchini Comoro.
Yanga na Comorozine wanatarajia kucheza
Februari 7, mwaka huu kwenye Dimba la Taifa jijini Dar ukiwa ni mchezo wa
kwanza na iwapo Yanga itafuzu itakutana na El Ahly ya Misri.
Okwi alisimamishwa na Kamati ya Sheria, Maadili
na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kucheza ligi mpaka
watakapopata ufafanuzi kutoka Fifa kama Yanga wanaweza kumtumia mchezaji huyo.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alisema tayari Shirikisho
la Soka Afrika (Caf), limemuidhinisha na wao wanafuata kauli hiyo na siyo ya
TFF kwa kuwa ligi hiyo siyo yao.
Alisema hawana hofu juu ya hilo kwa kuwa
Caf ni wakubwa kuliko TFF ambao wamekataa mchezaji wao asicheze kwenye ligi yao
kwa hiyo hawana hofu juu ya hilo.
“Sisi tumeruhusiwa kumtumia Okwi na Caf
kwa hiyo kwenye mechi yetu dhidi ya Comorozine ataanza kuonekana akiwa
uwanjani.
“Wao TFF si wamekataa tusimtumie kwenye
ligi yao, sasa Caf ni wakubwa zaidi yao na tutamtumia,” alisema Beno.
0 COMMENTS:
Post a Comment