Wakati mabeki wa timu nyingine za ligi
kuu hapa nchini wakisuasua kuzungumzia ubora wa mshambuliaji wa Simba, Ramadhan Singano ‘Messi’, beki wa kati wa Rhino
Rangers, Ladislaus Mbogo ameibuka na kusema kuwa mchezaji huyo kwa sasa ni zaidi ya Emmanuel Okwi na Mrisho Ngassa.
Mbogo ambaye aliwahi kuitumikia
Yanga msimu uliopita, alikumbana na
kashikashi za Messi katika mchezo wa ligi kuu uliozikutanisha timu hizo mbili kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam, Jumapili iliyopita na Simba
iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Bao hilo pekee la Simba katika mechi
hiyo lilifungwa na Messi baada ya kuwazidi ujanja Mbogo
pamoja na beki mwenzake, Laban Kambole.
Mbogo amesema kuwa amewahi kupambana na Okwi pamoja na
Ngassa lakini hakupata usumbufu mkubwa wa
kuwakaba kama alioupata kwa Messi, Jumapili iliyopita.
“Kama nisingekuwa makini ningeumbuka, ilinibidi nitumie
akili nyingi sana kumkaba, kuna wakati ilibidi nitumie nguvu ili
kumtisha apunguze kasi.
“Hivi sasa katika ligi kuu Messi ni zaidi ya Ngassa na Okwi, atakayebisha
ni mwongo,” alisema Mbogo.
0 COMMENTS:
Post a Comment