Na Saleh Ally
HII ni
miaka ya tabu kwa Manchester United, yaani 2013-14, hata kama kutakuwa na
marekebisho, basi ndiyo kipindi kigumu sana kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Timu yao
haifanyi vizuri na inaonekana wataalamu kadhaa wanakubaliana kwa hilo wakiamini
lazima kungekuwa na mtikisiko kutokana na kuondoka kwa Kocha Alex Ferguson
ambaye amedumu katika kikosi hicho kwa miaka 27.
Kuondoka
kwake lazima kuwe na mtikisiko, ndiyo maana kocha mpya, David Moyes amekuwa
katika wakati mgumu sana akionekana ni tatizo, kinda na maneno mengi
anayotupiwa, lakini uongozi umezidi kuonyesha unamuamini.
Hadi baada
ya mechi 20, Manchester United ambao ndiyo mabingwa watetezi wamebaki katika
nafasi ya saba wakiwa na pointi 34, tofauti ya pointi 11 na vinara Arsenal.
Marekebisho
yanawezekana, ingawa taratibu matumaini ya kuwa mabingwa tena yameanza kuyeyuka
taratibu, lakini kinachowatisha zaidi mashabiki wake ni hiki; hata wanapokuwa
nyumbani Old Trafford bado hawana uhakika wa ushindi.
Hawana
uhakika huo, kwani katika mechi 10 walizocheza nyumbani, Manchester United
wamepoteza nne, sare mbili na kushinda nne tu, hii si kawaida.
Si kawaida
na hasa kwenye ligi, ikitokea timu f’lani inakutana na Manchester United ndani
ya Old Trafford maarufu OT basi bora kulilia sare kwa kuwa jamaa kwao ni
‘wabaya’.
Lakini sasa
ni tofauti, mashabiki wake wamelalama kwamba wanaingia OT wakiwa ‘roho
mkononi’, hofu ya kupata presha hata kama wanacheza na timu inayoweza kuitwa
ndogo.
Mashabiki
hao wanasema bora wangekuwa hawapotezi nyumbani, angalau uhakika wa pointi za
OT, zingewapa ahueni lakini sasa hawajui wapi hasa Manchester United ina makali
hasa.
Rekodi ya
ugenini inaonyesha katika mechi 10, imeshinda 6, sare mbili na kupoteza 2.
Maana yake, Manchester United ya Moyes ni bora zaidi ugenini hata kuliko
nyumbani.
Hata katika
ufungaji, inaonyesha katika mechi 20 za nyumbani Manchester United, imefunga
mabao 12 tu na kufungwa 10, lakini ugenini imefunga 21 na kufungwa 14.
Hesabu
zinaonyesha Manchester United ikiwa ugenini imefunga mabao takribani mara mbili
ya yale iliyofunga nyumbani, kitu ambacho kiufundi si sahihi.
Wakati
rekodi nzuri kwa timu ni kuwa bora zaidi nyumbani kwanza, halafu kuhakikisha
unafanya kazi kwa uhakika kuzipata za nyumbani.
Maana yake,
kama Moyes atataka kurekebisha kikosi chake kianze kupata, lazima arekebishe
mwenendo wa OT. La sivyo, Manchester United itaendelea kufulia.
MABAO:
NYUMBANI
UGENINI JUMLA
Mabao
iliyofunga 12
21 33
Mabao
iliyofungwa 10 14 24
MECHI 8 ZA MWISHO:
P W D L Pts
Manchester City 8 7 1 0 22
Chelsea 8 6 1 1 19
Everton 8 5 2 1 17
Arsenal 8 5 2 1 17
Tottenham 8 5 2 1 17
Liverpool 8 5 0 3 15
Manchester Utd 8 4 1 3 13
MECHI ILIZOPOTEZA NYUMBANI:
Sept 28:
Man United 1 Vs West Brom 2
Des 4:
Man United 0 Vs Everton 1
Des 7:
Man United 0 Vs Newcastle 1
Jan Mosi:
Man United 0 Vs Tottenham 1
REKODI:
Mechi za nyumbani shinda 4, sare 2, poteza 4
Ugenini shinda 6, sare 2, poteza 2
0 COMMENTS:
Post a Comment