January 8, 2014




Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, amesema kwa sasa anaangalia zaidi viwango vya wachezaji wake vikoje katika michuano ya Kombe la Mapinduzi na hana presha na michuano hiyo kwani anaamini timu yake itafanya vyema kwa hatua iliyofikia.
 
Simba ambayo imefanikiwa kufika hatua ya robo fainali katika michuano hiyo ya Mapinduzi baada ya kuifunga bao 1-0 timu ya KMKM, imeonekana kubadilika kila siku zinavyokwenda mbele.

Akizungumza na Championi Jumatano, kocha huyo alisema kwa sasa anaangalia viwango vya wachezaji wake zaidi katika michuano hii ya Mapinduzi inayoendelea kwa sasa.

Loga alisema ni wakati mzuri kwa kuangalia uwezo wa wachezaji wake ili asiweze kupata shida katika upangaji wa kikosi cha kwanza katika timu hiyo ambayo ameanza kuifundisha hivi karibuni.

Aidha alisema katika michuano hii, hana presha na kikosi chake na anashukuru kwa kikosi chake kufikia hatua hiyo ya robo fainali ambapo anaamini timu itafika mbali japo mpira hautabiriki.

“Kikubwa kwa sasa naangalia uwezo na viwango vya wachezaji wangu viko vipi ili kuweza kuhakikisha wanafanya vyema si kwa Mapinduzi tu, hata katika michuano iliyopo mbele yetu.

“Sina presha, kikubwa ni kuhakikisha timu yangu inazingatia yale ambayo wanaelekezwa ili kuweza kufanikiwa wanapokutana na wapinzani wao katika mchezo na kuweza kufanya vyema,” alisema Loga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic