MWAMBUSI |
Kocha wa
Mbeya City, Juma Mwambusi amesema pamoja na kujua wamepaniwa sana kikosi chake
kimepania kuendelea ushindi.
Mwambusi,
amesema wanajua kila timu imepania kuvunja rekodi yao ya kutofungwa kwenye
ligi, lakini wataendelea kupambana.
“Kila mmoja
anataka kuwa wa kwanza kushinda dhidi ya Mbeya City, lakini na sisi tumepania
kuendeleza rekodi.
“Wachezaji,
benchi la ufundi na wote kwa ujumla tunalijua hilo, lakini tunaendelea
kupambana,” alisema Mwambusi.
Mbeya City
iliyoonekana huenda ni nguvu ya soda, ilirejea katika mzunguko wa pili wa Ligi
Kuu Bara kwa ushindi tena ikiilaza Kagera Sugar kwao Bukoka kwa bao 1-0.
Mechi yake
ya pili, ikapambana kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Ruvu kwenye Uwanja wa
Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
0 COMMENTS:
Post a Comment