Na Richard Bukos, Tanga
Mshambuliaji mpya wa Yanga, Emmanuel
Okwi, raia wa Uganda, ambaye amesimamishwa kutokana na suala lake la uhamisho
kuzua utata, jezi yake imeendelea kugombewa kama njugu na mashabiki wa timu
hiyo waliokutwa na Championi Jumatano maeneo ya Uwanja wa Mkwakwani mjini hapa,
jana Jumanne.
Yanga ipo mjini hapa kwa ajili ya mchezo
wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union utakaopigwa leo Jumatano.
Akizungumza na Championi Jumatano, mmoja
wa wauzaji wa jezi aliyejitambulisha kwa jina la Khalid Mwalimu, alisema katika
rundo la jezi anazouza, nyingi ni kama za kupamba biashara tu lakini jezi
inayouzika kama njugu ni ya Okwi.
"Hizi unazoziona nimezifuata mara
ya tatu, kila nikileta namaliza, nafuata nyingine, wengine wanachukua za Ngassa
lakini jezi za Okwi leo ndiyo zimekuwa dili sana.
“Mpaka huko tunakochukua mzigo wa jumla
nao wamesema wameshamaliza, wametuahidi labda kesho ndiyo wanaweza kutuletea nyingine,"
alisema Mwalimu kwa lafudhi ya kabila la Wadigo huku akiwa ameshika jezi hizo.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment