Timu ya Mgambo JKT ya jijini Tanga,
imeapa kukaza buti kuhakikisha inafanikiwa kutoshuka daraja msimu ujao kwa
kuhakikisha inashinda michezo iliyopo mbele yao.
Mgambo ndiyo timu inayoburuza mkia kufuatia
kuwa na pointi saba katika mechi 13 ilizocheza katika mzunguko wa kwanza.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mohammed Kampira, alisema wamejiandaa kuhakikisha timu
inafanya vizuri zaidi.
Alisema kufanya kwao vizuri ndiyo
kutawasaidia kutoka mkiani mwa ligi kuu na hatimaye kubaki kwenye ligi msimu
ujao.
“Maandalizi yanakwenda vyema na tumejipanga
ipasavyo kuhakikisha tunafanikiwa kushinda mechi zote za nyumbani ili kujiweka
katika nafasi nzuri.
“Wachezaji wangu wote wapo katika hali
nzuri ya kiushindani na majeruhi waliokuwepo hivi sasa ni wachache tu na hadi
mzunguko wa pili utakapoanza watakuwa fiti tayari kwa kuanza ligi,” alisema Kampira.
Mwishoo.
0 COMMENTS:
Post a Comment