January 31, 2014


Beki beki Shomari Kapombe atachota kitita cha dola 86,000 (zaidi ya Sh milioni 127) kwa mwaka kutoka Simba
.
Kapombe ambaye ana mkataba wa miaka miwili na Klabu ya AS Cannes inayoshiriki Ligi Daraja la Nne nchini Ufaransa, pia ameingia mkataba na Simba ambao utamwezesha kupata fedha hizo.
Katika mkataba huo na Simba uliosaini Agosti 19,2013 ambao gazeti hili lina nakala yake, kuna vipengele vinavyoonyesha Simba imekubali itampa Kapombe dola 50,000 (zaidi ya Sh 80)  kwa ajili ya usajili, mshahara wa dola 3,000 ambao kwa mwaka ni dola 36,000 (Sh milioni 57) ambazo zote jumla ni zaidi ya Sh milioni 137).
Kwa mujibu kati ya makubaliano kati ya Kapombe, AS Cannes na Simba, beki huyo atatakiwa kurudi Simba baada ya kumaliza mkataba wake Ufaransa na hasa akiwa hajauzwa na Msimbazi watamlipa fedha hizo za usajili pamoja mshahara wa dola 3,000 kila mwezi.
Nakala ya mkataba kati ya Kapombe na Simba inaonyesha uongozi wa Msimbazi umekubali kumlipa fedha hizo iwapo hatauzwa na AS Cannes, basi atarudi kuichezea Simba, lakini ikishindwa kumlipa mshahara na fedha hizo za usajili, Kapombe atakuwa huru kwenda anakotaka.

Kapombe bado amekwama nchini kutokana na mgogoro na AS Cannes baada ya kurudi nchini kuichezea Taifa Stars dhidi ya Zimbabwe, lakini baadaye iligundulika anadai mshahara na sasa inaelezwa ameishalipwa. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic