Mshambuliaji tegemeo wa Swansea, Wilfried Bony (pichani juu) amefunga
bao la ushindi na kuiwezesha timu yake kuibwaga Man United kwa mabao 2-1 katika
mchi ya Kombe la FA, leo.
Kwa kipigo hicho, Man United chini ya
David Moyes imeng’olewa kwenye michuano ya FA mapema kabisa.
Bonny ndiye alimfunga kipa nyota nchini
Juma Kaseja bao la nne wakati Ivory Coast iliposhinda kwa mabao 4-1 dhidi ya
Taifa Stars kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mwaka jana.
Man United pamoja na kuwa nyumbani
lakini ilishindwa kufurukuta na kuambulia bao moja lililofungwa Javier Harnandez
‘Chicharito’.
Beki Fabio alilambwa kadi nyekundu na
kuzidi kuongeza udhaifu kwa Man United.
Nayo Chelsea iliichapa Derby County kwa
mabao 2-0 na kusonga zake mbele, wafungaji ni Mikel Obi na Oscar.
MATOKEO MENGINE YA FA LEO.
Liverpool 2 Oldham 0
Nottingham 5 West Ham 0
Sunderland 3 Carlisle 1
0 COMMENTS:
Post a Comment