Simba imefanikiwa kutinga fainali ya
Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa URA ya Uganda kwa mabao 2-0.
Pamoja na kutinga fainali, Simba
imevunja mwisho wa kushindwa kuifunga URA kila zilipokutana na safari hii chini
ya Kocha Zravko Logarusic imeonyesha mambo tofauti.
Wauaji wa URA walikuwa ni beki wao wa
zamani, Joseph Owino na mkongwe Amri Kiemba ambaye ameng’ara tokea mwanzo wa
michuano hiyo.
Sasa Simba itacheza fainali ya michuano
hiyo Jumatatu dhidi ya KCC ya Uganda ambayo imeondoa na kuivua ubingwa Azam FC
katika fainali ya kwanza leo mjini Pemba.
Katika mechi hiyo ya Simba kwenye Uwanja
wa Amaan mjini Unguja, soka lilikuwa la ushindi lakini vijana wa Logarusic anayesaidiana
na Selemani Matola walionyesha wako fiti zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment