SIKILO 'MZARAMO', ENZI YA UHAI WAKE |
Sultan Sikilo aliyefariki dunia jana saa
7 mchana amezikwa leo katika makaburi ya Kibada, Kigamboni jijini Dar.
Sikilo, mwandishi mwandamizi wa michezo
na mweka hazina wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (Taswa), alifariki
dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Sikilo ambaye alijulikana kwa jina la
utani la Mzaramo au Mfano Mbaya kutokana na utani wa wachezaji wenzake wa
kikosi cha Taswa FC atakumbukwa kwa mengi ikiwa ni pamoja na uchapakazi.
Alikuwa kati ya waandishi wa mwanzo
kuliandikia gazeti la Bingwa akiwa na akina Saleh Ally, Hassan Bumbuli,
Selemani Mkangara na wengine.
MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA
PEPONI
0 COMMENTS:
Post a Comment