Yanga
SC wameanza mazoezi rasmi nchini Uturuki katika kambi yao ya wiki mbili.
Pamoja
na hivyo, Yanga wamepata bahati ya kukutana na beki wa zamani wa Real Madrid na
Brazi, Roberto Carlos.
Carlos
aliyekuwa maarufu kama mashuti sasa ni Kocha Mkuu wa timu ya Sivasspor inayoshiriki
Ligi Kuu ya Uturuki.
Carlos
aliungana na Yanga kwenye Uwanja wa Hoteli ya Sueno Beach Side nje kidogo ya
mji wa Antalya na kupiga picha na wachezaji pamoja na makocha wa timu hiyo,
Charles Boniface Mkwasa na Juma Pondamali.
Baada
ya hapo, Yanga waliendelea na mazoezi kujiandaa na lala salama ya Ligi Kuu Bara
pamoja na michuano ya Kimataifa kwa kuwa wao ndiyo wawakilishi wa Tanzania
katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment