January 28, 2014


Baada ya kupumzika jana, Kocha Zdravko Logarusic leo anakirudisha kikosi chake uwanjani kuendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar.


Wachezaji wa Simba jana walipewa mapumziko ya siku moja kabla ya kurejea mazoezini leo tena.
Logarusic amesema wanarejea mazoezini wakiwa wamelenga kufanya vizuri katika mechi ijayo dhidi ya JKT Pljoro ya Arusha.
“Mapumziko yanasaidia, sasa tunaanza tena kujiandaa na mpira kila siku maandalizi mapya na kujifunza upya,” alisema.
Simba imeanza vizuri mzunguko wa kwanza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rhino ya Tabora na mechi dhidi ya Oljoro itakuwa ni ya kuthibitisha kwamba hawajabahatisha.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic