YANGA NA COASTAL ZILIPOKUTANA TAIFA KWENYE MZUNGUKO WA KWANZA, SASA ZINAKUTAKA KESHO KATIKA MZUNGUKO WA PILI MJINI YANGA. |
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
inaendelea kesho (Januari 29 mwaka huu) kwa Coastal Union kuikaribisha Yanga
kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini.
Kiingilio katika mechi hiyo ni sh.
5,000 na sh. 15,000. Nayo Ruvu Shooting na Mbeya City zitapambana kwenye Uwanja
wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani kwa viingilio vya sh. 10,000 na sh.
5,000.
Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Kagera Sugar na Mtibwa Sugar. Viingilio ni
sh. 5,000 na sh. 3,000.
Azam itaumana na Rhino Rangers katika
Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Mbagala. Viingilio ni sh. 10,000 na sh.
3,000.
0 COMMENTS:
Post a Comment