Na Mwandishi Wetu, Tanga
Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga
wameuchangamsha mji wa Tanga kutokana na mechi ya kesho kuwa gumzo.
Pamoja na mashabiki wa Coastal Union
kujiamini kwamba kesho lazima Yanga ikae, lakini Yanga wanaonekana kujiamini
zaidi.
Katika sehemu mbalimbali za mji wa
Tanga, gumzo kubwa limekuwa ni namna mechi hiyo ya kesho itakavyokuwa.
Yanga tayari iko mjini hapa na
imefanya mazoezi huku ikionyesha kikosi chao kipo fiti na wanaisubiri Coastal
kwa hamu.
Gumzo la Uturuki na Oman ambako timu hizo ziliweka kambi pia limechukua nafasi kubwa.
Timu hizo mbili zote ziliweka kambi
nje ya nchi, Yanga ilisafiri hadi Uturuki, Coastal ikajificha nchini Oman
kujiandaa na Ligi Kuu Bara.
Yanga imeanza Ligi Kuu Bara mzunguko
wa pili kwa ushindi wa mabao 2-1 wakati Coastal Union ilishikiliwa na JKT
Oljoro ikiwa kwake Mkwakwani.
0 COMMENTS:
Post a Comment