KIPRE |
Straika wa Azam FC, Muivory Coast, Kipre
Tchetche, amesema uwepo wa Ismael Kone kwenye kikosi hicho ni ishara kubwa ya
kufanya vizuri zaidi kwenye safu ya ushambuliaji wa timu hiyo katika mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Kone ambaye pia ni raia wa Ivory Coast,
ametua Azam kwenye usajili wa dirisha dogo kuimarisha safu ya ushambuliaji ya
timu hiyo inayoshikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
Tchetche alisema kuwa wanaelewana kwa kiasi kikubwa wanapokuwa uwanjani na Kone
hivyo anaamini watafanya makubwa kutokana na uchezaji wao huo.
Alisema kuwa uwezo wa kiungo huyo
mshambuliaji ni mzuri na ni mchezaji ambaye hahofii mabeki na huwa anajitahidi
kufanya analoweza ili mradi ahakikishe anaipa ushindi timu yake, kitu ambacho
kina faida kubwa kwa Azam.
“Kone ni mchezaji mzuri anayeyajua
majukumu anapokuwa uwanjani, kwa hiyo mtu kama huyu unapofanya naye kazi
inakuwa ni rahisi sana kufanikisha mnalolitaka kwa timu ambalo ni ushindi
pekee, naamini pamoja tutafanya vizuri mzunguko wa pili,” alisema Tchetche.
0 COMMENTS:
Post a Comment