Yanga imeanza vizuri kambi yake ya mazoezi nchini Uturuki
baada ya kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Ankara Sekerspor katika mechi
ya kirafiki iliyochezwa leo mjini Antalya.
Mabao ya Yanga katika mechi hiyo yalifungwa na wachezaji
watatu wa kimataifa, Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi (wote raia wa Uganda) na Didier
Kavumbagu raia wa Burundi.
Mechi hiyo ilikuwa na upinzani mkali kutokana na wenyeji hao
kutumia nguvu zaidi na pia muonekano wa maumbo yao.
Lakini wachezaji wa Yanga walionekana kucheza mpira wa
chinichini na pasi za haraka na kuwadhibiti vilivyo hadi walipoanza
kuwadondoshea bao moja moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment