January 24, 2014





Hati ya Usajili wa Emmanuel Okwi kama inavyoeneka kwenye system ya CAF.
Uongozi wa klabu ya Young Africans umeamua kuweka hadharani ukweli kuhusiana na usajili wa mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi ambaye kamati ya maadili na hadhi za wachezaji imemzuia kuichezea Young Africana mpaka watakapopata uthibitisho kutoka FIFA.


Young Africans ilikamlisha usajili wa mshambuliaji huyo tangu Disemba 15 mwaka 2013, na kupata hati ya uhamisho wake wa kimataifa (ITC) ambayo iliwasilishwa TFF pamoja na fomu mama za usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Baada ya kukamilisha zoezi hilo TFF ilipitisha jina lake kwa kutupatia leseni no: 921225001 ambayo inamruhusu mchezaji kuichezea Young Africans na kisha kulituma CAF Disemba 31, 2013 kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika  ambapo CAF nao walimuidhinisha kuwa mchezaji halali wa Young Africans kwa mashindano hayo.
Cha kustaajabisha siku mbili kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Kamati ya Maadili na hadhi za wachezaji wakamzuia mchezaji huyo kuichezea Young Africans ilihali akiwa ameshaidhinishwa na TFF na CAF kuwa mchezaji halali wa Young Africans.
Swali?? walikuwa wapi Kamati ya Maadili na Hadhi za Wachezaji kujiridhisha juu ya usajili ambao ulishakamilika tangu Disemba 15 2013?
Wanakuja kutoa maamuzi hayo mwezi mmoja na nusu baada ya dirisha la usajili kufungwa, ikiwa ni siku mbili kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom??

5 COMMENTS:

  1. tff matako matupu wanafanya kzi kwa hisia

    ReplyDelete
  2. ndio mnatukwamisha mpira wetu kuendelea, magumashi mengi sijui ni vipi mi naskia hasira sana, hivi wanajua kazi yao? malinzi anakazi kubwa sanaaaa, kuna uwozo umebaki pale washenzi watupuuuuuuuuuuuuuu kum* nin* zenu. magumashi tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  3. Inashangaza kuwa viongozi wa Yanga wanatoa liseni ya CAF Kama uthibitisho wa uhalali wa usajili wa huyu mchezaji. Mkumbuke T P Mazembe walinyang'anywa ushindi baada ya Simba kuwakatia rufaa juu ya mchezaji mmoja ambao wao walimsajili kama mchezaji huru wakati kumbe alikuwa ni wa Etoile hii hii ya Tunisia. Hizi liseni hutolewa kwa maelezo ya timu inayoomba na Kama maelezo ni ya uwongo bado watapata hizo liseni lakini wakigundulika ndiyo hayo ya kupokwa ushindi na adhabu zinginezo. Yanga waishukuru TFF kuwaokoa na janga hilo maana ruhusa ikitoka FIFA kutakuwa hakuna tatizo. Yanga, Villa na FUFA wote wanadai waliruhusiwa na FIFA lakini wakiulizwa wapi uthibitisho huo hawautoi sasa hii ndio magumashi na TFF ikaona ijiridhishe kwa kuulizia hilo sasa pana ubaya gani? Kuchelewa kwa uamuzi kulisababishwa na yule afisa aliyetoa ITC kutoweka bayana vielelezo via FIFA ili ionekane kuwa mambo yote ni sahihi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic