BOSI WA TPLB, YAHAYA |
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
imetoa sh. milioni 1.5 kwa kila klabu ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Uamuzi wa kuzisaidia timu hizo
ulifanywa katika kikao cha TPLB kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es
Salaam ambapo fedha hizo zitalipwa kupitia kwenye akaunti za klabu husika.
Hivyo klabu ambazo hazijawasilisha akaunti zao TPLB zinatakiwa kuwasilisha haraka.
Klabu za FDL ni African Lyon, Burkina
Moro, Friends Rangers, Green Warriors, Kanembwa JKT, Kimondo, Kurugenzi
Mafinga, Lipuli, Majimaji, Mkamba Rangers, Mlale JKT na Mwadui.
Nyingine ni Ndanda, Pamba, Polisi Dar
es Salaam, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Morogoro, Polisi Tabora, Stand
United, Tessema, Toto Africans, Trans Camp na Villa Squad.
0 COMMENTS:
Post a Comment