Uongozi wa
Etoile Du Sahel ya Tunisia kwa mara ya kwanza umetoa taarifa ambayo haikuwahi
kutolewa kuhusiana na mshambuliaji, Emmanuel Okwi kwa kusema alitoroka
‘kimafia’ nchini Tunisia na kusema ilikuwa kama sinema.
Etoile
wamesema Okwi alizuiwa kwenda kuichezea timu ya taifa ya Uganda iliyokuwa
inaivaa Liberia, lakini aliamua kutoroka bila ya taarifa yoyote kwa kiongozi au
mchezaji yeyote.
Akizungumza
na SALEHJEMBE kutoka mjini Sousse, Tunisia jana, Ofisa Utawala wa
Etoile aliyejitambulisha kwa jina moja la Amra, alisema wameshangazwa na tabia
za Okwi na hawajawahi kuona.
“Ilikuwa
kama sinema kabisa, kwetu kilikuwa ni kitu cha ajabu, hadi leo hapa ni gumzo
kwa kuwa haijawahi kutokea. Okwi hakutakiwa kuondoka hapa Sousse na kwenda
Uganda na hata alipoondoka hatukujua hadi siku iliyofuatia.
“Tulijua
timu yake ina mechi muhimu, lakini alikuwa anapewa adhabu kwa kuwa akiondoka
anachelewa kurudi. Hivyo kulikuwa na mjadala kati yetu na Shirikisho la Soka Uganda
(Fufa), kama tungeelewana, basi angeondoka.
“Lakini akatoroka,
hatukujua hata aliondoka vipi. Suala lake limefika Fifa lakini sisi sidhani
kama tutakuwa tunamhitaji, ila tunasubiri mambo kadhaa yafikiwe halafu tutatoa
tamko,” alisema.
Okwi ambaye
alipata kibali cha kuichezea SC Villa ya Uganda kwa miezi sita kabla ya
kusajili Yanga, amegoma kurejea Tunisia kwa madai ya kutolipwa mshahara wake.
Wiki
iliyopita, uongozi wa Etoile ulisema haukutuma jina la Okwi kwenye Shirikisho
la Soka Afrika (Caf) kwa kuwa haukuona kama ni sahihi kwa vile wana mgogoro na
Okwi.
Lakini Kamati
ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF, imesimamisha usajili wake
Yanga kwa kuwa kuna kesi kati yake na Etoile na pia Etoile na Simba.
Okwi yuko
nchini, lakini kesho atakosa mechi ya pili wakati Yanga ikisubiri taarifa kutoka
Fifa na tayari TFF imeishaandika barua.
0 COMMENTS:
Post a Comment