January 8, 2014





Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, juzi alimpanga kwa mara ya kwanza kipa wake mpya, Yaw Berko ambaye aliibuka kivutio kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya KMKM.


Katika mchezo huo ambao mashabiki walikuwa wakimshangilia kipa huyo kwa nguvu kubwa dakika zote alizokuwa uwanjani, Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutinga robo fainali.

Kipa huyo aliweza kuchukua nafasi ya Ivo Mapunda ambaye amekuwa akicheza kwenye michezo mingi ya timu hiyo, lakini aliweza kuonyesha kiwango cha juu kwa kuokoa michomo mikali.

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amani mjini Unguja, ulihudhuriwa na mashabiki wengi ambao walikuwa wakishangilia muda wote.

Simba iliweza kuutawala mchezo huo na kujipatia bao la mapema lililofungwa na Amri Kiemba katika dakika ya nne ya mchezo.

Hata hivyo, Loga alifanya jambo ambalo lilishangiliwa, ni baada ya kuwaanzisha wachezaji watatu Wazanzibar katika mchezo huo, jambo ambalo alisema ni kwa kuwa wana uzoefu na timu za huko.

Aliwaanzisha Abdulhalim Humud, Ali Badru na Adeyum Saleh ambao wote ni wazaliwa wa Zanzibar.

Kwa matokeo hayo Simba sasa inatarajiwa kuingia uwanjani leo kuvaana na Chuoni ya Zanzibar katika mchezo wa robo fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic