Madakatri wote wa timu za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) kupitia klabu zao wanatakiwa kuwasilisha vyeti pamoja na wasifu
wao (CV) kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufikia Februari 8
mwaka huu.
Wasifu na vyeti hivyo vinatakiwa ili
kuwezesha Kamati ya Tiba ya TFF kuandaa mafunzo kwa wataalamu hao wa tiba kwa
wachezaji.
Pia TFF itatoa kwa madaktari hao fomu
maalumu za vipimo kwa wachezaji ambapo kila mchezaji atatakiwa kufanyiwa vipimo
vyote kama ambavyo fomu imeelekeza.
Hakuna mchezaji atakayeruhusiwa
kuendelea kucheza VPL au kuchezea timu za Taifa kama atakuwa hajafanya vipimo
hivyo. Machi 1 mwaka huu ndiyo utakuwa mwisho wa kurejesha fomu za vipimo vya
wachezaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment