MSAFARA WA YANGA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA KITAMAIFA WA JULIUS NYERERE, LEO ALFAJIRI |
Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga leo
wameondoka jijini Dar es Salaam saa 10:35 alfajiri kwenda Antalya nchini
Uturuki.
Yanga itaweka kambi Antalya kwa kipindi
cha zaidi ya siku kumi na inatarajia kuwasilia Istambuli leo asubuhu na mchana
itaunganisha ndege kwenda Antalya.
Yanga imeondoka na kikosi cha jumla ya
wachezaji 27, jumla ni watu 33 ukijumlisha benchi la ufundi na kiongozi wa
msafara Bwana Rupia.
Kocha Msaidizi, Charles Boniface Mkwasa
ndiye aliongoza msafara kwa upande wa benchi la ufundi akisaidiana na kocha wa
makipa, Juma Pondamali.
Hii ni mara ya pili kwa Yanga kuweka
kambi katika mji huo lengo likiwa ni kujiimarisha kwa ajili ya mzunguko wa
lalasalama wa Ligi Kuu bara.
Hivi karibuni, Yanga ilimtimua kocha
wake Ernie Brandts na sasa iko kwenye mchakato wa kusaka kocha mpya.
0 COMMENTS:
Post a Comment