Wekundu wa Msimbazi Simba wametinga nusu
fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Chuoni ya Zanzibar kwa mabao
2-0.
Mrundi Amissi Tambwe na kinda Ramadhani
Singano ‘Messi’ ndiyo waliofanya ‘mauaji’ hayo usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan
mjini Zanzibar.
Simba chini ya Kocha Zravko Logarusic na
msaidizi wake Selemani Matola ilionyesha soka la kuvutia na kuwapa wakati mgumu
Chuoni.
Pamoja na kuonyesha juhudi lakini wakati
fulani, Chuoni walilazimika kuutafuta kwa tochi ili kupambana na makali ya Simba
ambao walionekana wako sawa.
0 COMMENTS:
Post a Comment