Beki wa Yanga, David Luhende, amesema
anafurahi baada ya kocha wake, Hans van Der Pluijm, kumpanga namba 11.
Katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu ya
Tanzania Bara, Luhende alicheza namba hiyo badala ya beki wa pembeni ambayo
alikuwa akicheza awali.
Luhende alianza kucheza namba 11 katika mechi ya kwanza ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ashanti United.
“Nimefarahi kuicheza nafasi hii ya kiungo
mshambuliaji ambayo zamani ndiyo nilikuwa naichezea, lakini nilibadilishwa na
kuwa beki kipindi fulani lakini nitajitahidi ili kuweza kuendelea kuimudu
vizuri.
“Nitajituma zaidi kuhakikisha timu yangu
inafanya vyema mzunguko huu, japo bado ushindani unaonekana ni mkubwa sana
katika ligi lakini inabidi kujituma ili tuweze kufanya vizuri,” alisema
Luhende.
0 COMMENTS:
Post a Comment