Kweli Al Ahly ni janja ya nyani, kwani pamoja na kupoteza mechi
kadhaa za Ligi Kuu Bara, imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Super Cup.
Al Ahly imetwaa ubingwa huo kwa
kuichapa CS Sfaxien ya Tunisia kwa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa jijini Cairo huku
Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa akishuhudia live.
Mkwasa alikuwa uwanjani hapo kukamilisha
idadi ya mashabiki 30,000 waliokubaliwa na serikali ya Misri kuingia uwanjani
hapo.
Kocha huyo na mchezaji wa zamani wa
Yanga, aliongozana na Watanzania waliokuwa tayari kuisaidia Yanga kwa ajili ya
utaifa na baadhi ya maofisa wa ubalozi.
Ben Youssef aliifungia Sfaxien katika
dakika ya 12 na kuamsha dalili za ushindi kwa wageni lakini mshambuliaji wa zamani wa Hull City, Mohamed
'Gedo' Nagy akaisawazishia
Amr Gamal akapiga bao la pili kwa Sfaxien katika dakika ya 54
baada ya mkongwe wa Ahly Wael Gomaa kucheza faulo.
Mzaliwa wa Cameroon, Moussa Yedan alipiga krosi safi kwa Gamal
aluyepiga kichwa na kuisawazishia Ahly.
Baada ya bao hilo ilionekana kama Sfaxien
hawana ujanja na kutoa nafasi kwa Al Ahly kwenda mwendo wa nyuki na kufanikiwa
kupata bao la ushindi.
Mara ya mwisho Ahly ilikutana na Sfaxien,
miaka mitano iliyopita katika kombe hilohilo la Super Cup, wazee wa Cairo wakashinda.
Kocha Mkuu wa Ahly, Mohamed Youssef
alisema sasa wanarudisha nguvu kwenye ligi kwa kuwa wamepoteza mechi tatu
katika mechi tisa walizocheza.
0 COMMENTS:
Post a Comment