February 21, 2014


Uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), umesema kuwa hautavumilia kuona wafanyakazi na wanachama wake wakivunja taratibu na kanuni ilizojiwekea, kwa faida ya maslahi yao binafsi.


Hatua hiyo ya TFF imekuja ikiwa ni siku chache baada ya shirikisho hilo kumlalamikia mfanyakazi wake mmoja katika Kamati ya Maadili kutokana na kufanya udanganyifu katika suala la usajili wa mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi.

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa siku zote wamekuwa wakiwataka watu kuzingatia taratibu na kanuni za shirikisho hilo lakini baadhi yao wamekuwa wagumu kuzifuata.

“Kweli kabisa watu wamekuwa wakivunja taratibu na kanuni za TFF bila kujali.

“Kuanzia sasa tutakuwa wakali na tutahakikisha tunawachukulia hatua kali za kinidhamu wale wote watakaobainika kuzivunja, lengo letu ni kutaka kuona soka letu linapiga hatua zaidi,” alisema Wambura.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic