Mabingwa wa Afrika,
Al Ahly, wameishusha AC Milan ya Italia katika cheo cha kuwa timu yenye
makombe mengi zaidi ya kimataifa.
Al Ahly ambao ni
mabingwa wa Afrika, wanakutana na Yanga Jumamosi hii jijini katika mechi ya
Ligi ya Mabingwa inayosubiriwa kwa hamu jijini Dar.
Ushindi wa Al Ahly
dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia katika fainali ya Super Cup, umeifanya kufikisha
makombe 19 na kuivuka AC Milan na Boca Junior ambazo zina 18.
Uongozi wa Al Ahly,
tayari umetuma barua kuitaka AC Milan kuondoa maneno yaliyo kwenye nembo yake
yaliyoandikwa kwa lugha ya Kiitaliano “il club piu titolato al mondo”, ikiwa na maana, timu
yenye vikombe vingi vya kimataifa kuliko zote duniani.
Vikombe
hivyo vya Al Ahly; vinane ni vya Ligi ya Mabingwa, vinne ni Kombe la Washindi,
sita vya Super Cup na kimoja cha Afro-Asian cup.
Al
Ahly ina maanisha sasa ndiyo yenye vikombe vingi zaidi vya kimataifa, sifa ambayo
haijawahi kushindwa na timu yoyote ya bara la Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment