February 24, 2014


Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, Tom Olaba, juzi alifanya kituko cha mwaka baada ya kuliacha benchi na kwenda kujisaidia.


Kocha huyo alifanya jambo hilo wakati timu yake ikiwa nyuma kwa mabao 6-0 wakati ilipokuwa ikivaana na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mchezo ambao ulimalizika kwa Yanga kushinda 7-0.

Olaba ambaye muda mwingi wa mchezo huo alikuwa amesimama, aliondoka taratibu kwenye benchi la timu yake akaelekea vyumbani ikiwa ni dakika ya 75 ya mchezo huku mashabiki wakimzomea.

Kocha huyu raia wa Kenya akiwa vyumbani timu yake ilifungwa bao la saba, ambalo liliwekwa kimiani na Simon Msuva, huku kukiwa hakuna mtu hata mmoja aliyesimama kwenye benchi.

Zikiwa zimebaki dakika tano kocha huyo alirejea kwa madaha na kukuta timu yake imelambwa bao la saba.

“Mimi nilikwenda ‘toilet’, kwani nikiwa kocha sitakiwi kujisaidia?” alihoji kocha huyo mwenye mbwembwe na kuongeza:

“Niliwahi kumuona hata rais akitoka na kwenda kujisaidia, kwa nini kwangu ionekane ajabu?”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic