Aliyewahi kuwa kipa wa Simba na Ashanti
United, Amani Simba, anatarajiwa kuondoka nchini leo Jumatano kuelekea Nampula
nchini Msumbiji kwa ajili ya majaribio ya wiki moja.
Awali, Amani aliwahi kuliambia gazeti
hili kuwa amestaafu soka lakini sasa amesema kuwa ameamua kurejea tena kwa kuwa
ameona mwili wake bado una nguvu.
Amani
amesema anakwenda huko kwenye majaribio
hayo akiamini kuwa atafuzu kutokana na kwamba anaamini yeye bado ana kiwango na
atafanya vyema.
Alisisitiza anakwenda huko akiwa na
matumaini makubwa kuwa atafanikiwa.
“Siku ya Jumatano (leo), ninaondoka hapa
nchini kuelekea Nampula nchini Msumbiji kwa ajili ya majaribio, bado wakala
wangu hajanieleza ni timu gani lakini amesema inashiriki ligi kuu ya huko.
“Ninaamini nitafuzu kwa sababu bado nina uwezo
wa kufanya vizuri kutokana na kiwango changu na nimeamua kurejea upya katika
soka na ninakwenda kuanzia nje halafu nitarudi tena hapa nyumbani,” alisema
Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment