KIM AKIWA NA TASSO MUKEBEZI |
Kocha Mkuu
wa Taifa Stars, Kim Poulsen, amesifia kiwango cha timu changa kwenye ligi kuu,
Mbeya City na kusema kuwa ndiyo timu iliyopo kwenye kiwango cha juu zaidi kwa
sasa.
Kim amesema
katika mechi alizofuatilia, Mbeya City ndiyo imekuwa kwenye kiwango zaidi huku
timu nyingine zikitetereka katikati mwa msimu.
Kim alisema timu hiyo ni mfano wa kuigwa kwa timu zenye
ndoto ya kupata mafanikio na kuuza wachezaji kama zilivyo Simba na Yanga.
“Mbeya ni
mfano wa kuigwa, kwa maoni yangu ndiyo timu bora msimu huu. Wanacheza soka zuri
na la kuvutia wala hawajatetereka licha ya kuwa ni timu changa.
“Ni mfano
mzuri wa kuigwa kwa timu zinazotaka mafanikio na pia kuweza kuuza wachezaji kwa
timu kubwa hapa nchini au nje ya nchi kama zilivyo Simba na Yanga,” alisema
Kim.
Alipoulizwa
licha ya kiwango chao, iweje hakuna mchezaji wa City katika kikosi cha Taifa
Stars, Kim alisema: “Tuliita wanne
kwenye Future Young Taifa Stars, lengo lilikuwa kuangalia uwezo wao,
ukweli wana uwezo lakini wanakosa uzoefu, hivyo sikuweza kuwajumuisha kwenye
timu iliyokwenda Kenya kwa kuwa tulikuwa tunapigana vita kuhakikisha tunarudi
na chochote.
“Naamini
awamu ijayo, kutakuwa na wachezaji wengi wa Mbeya City kutokana na jinsi
wanavyocheza.”
Stars
inakabiliwa na mchezo mgumu wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya Shirikisho la
Soka la Kimataifa (Fifa), Machi 5 mwaka huu, kwa kuchuana na Namibia mjini Windhoek.
0 COMMENTS:
Post a Comment