Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Azam, Stewart
Hall, raia wa Uingereza, ameibuka na kuielekeza Yanga cha kufanya kama kweli
inataka kuiondoa Al Ahly ya Misri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga inatarajiwa kuumana na mabingwa
hao watetezi kwenye mchezo wa hatua ya pili ya michuano hiyo baada ya kuifunga
Komorozine ya Comoro kwa jumla ya mabao 12-2.
Hall alisema kwamba ni lazima Yanga
ishinde kwenye mchezo wa kwanza utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar kwa idadi
nyingi ya mabao kwa ajili ya kupunguza mzigo watakapokwenda kwenye mechi ya
marudiano.
Alisema kuwa endapo Yanga itafanikiwa
kufanya hivyo itakuwa na faida kwa kuwa mara nyingi Waarabu hao ni wagumu
kuwafunga wakiwa kwao, hivyo hata wakijitahidi kupata matokeo ya sare yoyote
itaweza kuwasaidia.
Aidha, aliwasihi pia kuwa waangalifu na
makini kwa timu hiyo ambayo ni ngumu hapa Afrika huku akiwataka watumie nafasi
hiyo kwa ajili ya kujitangaza zaidi hapa Afrika na sehemu nyingine duniani
kote.
“Yanga wanakutana na timu ngumu, cha
msingi ni kujipanga zaidi kwenye mechi hii ya kwanza ya nyumbani, inabidi
wapate ushindi mzuri kwa sababu kila mtu analijua hilo kwamba Al Ahly ni wagumu
kuwafunga kwao, wakiweza kufanya hivyo watakuwa na faida kubwa.
“Lakini pia wawe makini kwa vitu viwili,
kwanza wawe makini sana na hawa jamaa kwani
hawatabiriki kabisa wanapokuwa uwanjani, lakini pia ni muda wao muafaka
wa kujitangaza kwa sababu hizi timu za Kaskazini mwa Afrika huwa zinafuatiliwa
sana Ulaya, hivyo endapo itafanya vema itakuwa faida nyingine tena kwao na mchezaji
mmoja-mmoja,” alisema Hall.
Ivi wewe Iyo Habari HALL na YANGA Kuna Cha maana kweli Ulichoandika Kulinga na na Heding yako? Tunaacha Habari za Kijinga brbrn na Huku nako Tunazikuta hizo hizo
ReplyDeleteEti Awapa Mbinu..... Mbinu ndo Kuwaambia Waingalie iyo timu ni ngumu sana na Wachukue nafasi iyo Kujitangaza? Ivi Ulikuwa Seriouz Unaandika Hii hbr? Umeniangusha sana
ReplyDelete