Baba mzazi wa kiungo wa Simba, Amri Kiemba, Seif Athuman Kiemba,
amefunguka na kutaja siri ya kiwango kizuri cha mwanaye kwa sasa ambapo amesema
ni baada ya kumkalisha kitako na kumkanya.
Kiemba alipata wakati mgumu msimu uliopita kutokana na kuonekana kama
kiwango chake kimeshuka wakati timu hiyo ilipokuwa chini ya Kocha Abdallah
Kibadeni lakini sasa amekuwa akipata nafasi chini ya Kocha Zdravko Logarusic.
“Niliamua kumkalisha chini baada ya kuona kiwango chake kilikuwa chini
mno wakati wa Kibadeni kwenye kikosi cha Simba, ukweli alinielewa ndiyo maana
utamuona kwa sasa anacheza vizuri na kocha anamuamini,” alisema mzee Athuman,
mfanyabiashara maarufu hapa nchini.
Kiemba amekuwa akibadilishiwa namba na mara nyingine akikabidhiwa
kitambaa cha unahodha katika kipindi hiki ambapo Nassor Masoud ‘Chollo’
anauguza jeraha la mguu.
0 COMMENTS:
Post a Comment