February 21, 2014


Kocha Mkuu wa Simba, Mcrotia Zdravko Logarusic, amesema iwapo ataendelea kukinoa kikosi hicho msimu ujao, ndoto ya usajili wake ni kuchota nyota kutoka Ligi Kuu ya Kenya, kwani kuna wachezaji wenye uwezo mzuri na wenye kuendana na weledi wa kisoka (professionalism).


Loga ambaye aliwahi kufundisha soka nchini humo akiwa na Klabu ya Gor Mahia, alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na vipaji vya soka lakini hawana weledi, ndiyo maana wanampa tabu kufundisha.

Alienda mbali na kusema kuwa katika kipindi alichokaa Tanzania, hajaona mchezaji mwenye uwezo wa kucheza ligi kubwa hasa Ulaya kulinganisha na Wakenya waliosambaa kila kona ya dunia.

“Wachezaji wa Kenya ni waelevu, wanaelewa nini kocha anachotaka tofauti na hapa. Ndiyo, Tanzania kuna vipaji, lakini wachezaji wake siyo welevu, ndiyo maana wananisumbua hata katika ufundishaji.

“Kama kweli nitakuwa hapa msimu ujao, nitaleta wengine kutoka kule,” alisema Loga huku akiisifia Gor Mahia kuwa ina wachezaji wazuri.

Loga ambaye mkataba wake unakwisha Mei, mwaka huu, baada ya kufika Simba aliwasajili Ivo Mapunda ambaye ni Mtanzania aliyekuwa akicheza soka Kenya na beki Mkenya Donald Musoti.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic