Wanachama wa Yanga sasa watanufaika na mfumo mpya kwa kutumia kadi maalum za kutolea
fedha maarufu kama ATM, kama kadi za uanachama.
Habari za
uhakika kutoka Benki ya Posta zimeeleza kuwa, benki hiyo iko katika mchakato wa
mwisho kuidhamini Yanga na moja ya kazi zake itakuwa hiyo.
“Unajua
tumezungumza na uongozi wa Yanga, ikiwezekana mchakato huo pia tutafanya na
viongozi wa Simba. Lakini wanachama wa Yanga sasa watatumia kadi za Benki ya
Posta kama kadi za uanachama.
“Kila wiki
watakuwa wanakatwa kiasi fulani cha fedha kulipia ada yao, kitakuwa cha chini
sana na huenda mwanachama asisikie maumivu kabisa.
“Si unajua
kwa mwaka wanalipa Sh 12,000. Kwa mwezi ni shilindi elfu moja. Sasa jiulize kwa
wiki atakatwa shilingi ngapi? Huu utakuwa ni utaratibu mpya na wa aina yake.
“Kadi ya
uanachama na mwanachama ataweza pia kuhifadhia fedha zake kama anavyofanya
katika akaunti zake benki,” kilieleza chanzo hicho kutoka katika benchi hiyo.
Iwapo
itaanza, mpango huo utakuwa wa kwanza na wa aina yake kwa klabu za Tanzania
ambazo ulipaji wa ada za wanachama wake umekuwa wa kusuasua.
Yanga na
Simba ndiyo klabu zenye mashabiki wengi zaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki
na Kati lakini zimekuwa zikiteketea na umaskini kwa kuwa hakuna ubunifu.
0 COMMENTS:
Post a Comment