February 24, 2014


Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amekataa kwamba alilikimbia gari lake aina ya Toyota GX 110 na kupanda basi la wachezaji.


SALEHJEMBE ilimshuhudia Logarusic akiachana na gari hilo na kukwea basi la wachezaji ikiwa ni dakika chache baada ya mechi dhidi ya JKT Ruvu kwisha, huku Simba ikiwa imelala kwa mabao 3-2.
Logarusic alisogea karibu na gari lake, huku ikionekana kama mtu ambaye machale yamemcheza aliondoka na kupanda basi.
Wachezaji wa Simba pamoja nay eye, walitoka uwanjani hapo kwa kusindikizwa na magari ya jezi la polisi.
“Kweli nilipanda basi, lakini sikuwa ninakimbia. Hakukuwa na sababu ya kufanya hivyo.

“Nilitaka kujua ndani ya basi wachezaji wangu wanaendeleaje na kama kila kitu kinakwenda vizuri,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic