February 23, 2014


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm amesema ikiwezekana kushinda mabao mengine saba, litakuwa jambo zuri.


Yanga iliweka rekodi mpya ya mabao katika Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya jana kuibutua Ruvu Shooting kwa mabao 7-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara, jana.
Mholanzi huyo amesema anapenda kuona kikosi chake kinashinda mabao mengi zaidi.
Lakini akasisitiza, kama litatokea suala la kushinda mabao saba litakuwa safi zaidi.
“Ikiwezekana itakuwa vizuri zaidi, ikishindikana basi ushindi ni jambo zuri zaidi hata kama ni mabao mawili,” alisema.
Kocha huyo aliyefanya kazi nchini Ghana kwa mafanikio, amesisitiza kikosi chake kitaendelea kufanya vizuri zaidi.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic