LOGARUSIC ATOA MBINU ZA KUREKEBISHA
MWENDO
Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic
amesema moja ya njia ya kufanya vema kwa kikosi chake ni wachezaji wake kukataa
makosa zaidi.
Kocha huyo raia wa Croatia amesema
makosa makubwa wanayoyafanya ndiyo yamekuwa yakiwa mwelekeo mbaya katika ligi
hiyo.
“Kukosea mkaruhusu mkafungwa au kukosea
mkakubali kupoteza nafasi ya kufunga, tayari hilo ni kosa na mnakuwa mmejiondoa
njiani.
“Kama unapata nafasi unatumia, au
walinzi hawatoi nafasi ya timu pinzani kufunga, basi njia ya kufanya vizuri ni
lahisi kabisa.
“Wachezaji wangu ninazungumza nao sana,
lakini najua ni suala la kurudia na kurudia tena ili watu waelewe.
“Tumezunguka mikoani na kuambulia pointi
mbili tu, si sahihi na lazima tukatae kwamba huo si mwendo mzuri unaotufaa
sisi,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment