Kocha Mkuu wa Ruvu JKT, Fred Felix
Minziro amesema kupoteza mechi kwa mabao 6-0 dhidi ya Prisons haina maana
watakuwa laini dhidi ya Simba.
Kikosi cha Minziro kinakutana na Simba
kesho baada ya siku chache kupokea kipigo cha mabao 6-0 dhidi ya Prisons ya
Mbeya.
Minziro aliyekuwa kocha msaidizi Yanga
kabla ya kurejea JKT amesema kila mchezo unajitegemea na lengo lao ni kufanya
vizuri pia kujifunza kupitia makosa.
“Tunachotaka ni kufanya vizuri,
wachezaji wanajua tumepoteza na kuna makosa tulifanya. Hivyo hatupaswi kupoteza
tena.
“Tunatakiwa kurekebisha mambo wakati
tunakutana na Simba, tumejiandaa na tunaendelea kujiandaa. Watu wasidhani
itakuwa mechi lahisi,” alisema Minziro.
0 COMMENTS:
Post a Comment