Wayne Rooney noma, sasa amesaini mkataba mpya na Manchester United ambao utambakiza katika klabu hiyo hadi mwaka 2019.
Mkataba huo pia umevunja rekodi kwa kuwa moja ya mikataba
ghali zaidi kwa kuwa atakuwa akilamba pauni 300,000 (Sh milioni 750), kwa wiki huku kimuacha
Sergio Aguero anayechukua pauni 200,000 kwa wiki pia.
Rooney kusaini mkataba huo mpya ni sawa na ushindi kwa Kocha
David Moyes ambaye, jana amesema klabu hiyo haijawahi kuwa na mpango wa kumuuza
Rooney.
Chelsea walifikia kutoa hadi pauni milioni 30 mwishoni mwa
msimu uliopita wakimtaka Rooney baada ya taarifa kuzagaa hakuwa akielewana tena
na kocha aliyepita, Alex Ferguson.
Katika mkataba huu mpya, kuna kipendegelea cha Rooney
maarufu kama Wazza kuwa balozi wa Manchester United, mara tu atakapostaafu
soka.
0 COMMENTS:
Post a Comment