WAHUSIKA katika masuala ya ufundi ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ndiyo wanaokaa na kupanga ratiba ya Ligi Kuu
Tanzania Bara.
Namna ya ligi inavyochezwa ni nyumbani
na ugenini, lakini mambo yanakwenda hivi; mechi zinachezwa kwa mizunguko
miwili. Nyumbani na ugenini.
Mfumo huo ni duniani kote, lakini hapa
nyumbani inakuwa hivi, kama katika mzunguko wa kwanza Simba ilianza na Ruvu
Shooting, basi katikat mzunguko wa pili, vivyo hivyo itaanza tena na timu hiyo.
Sidhani kama ni sahihi sana, ingawa si vibaya.
Lakini katika upangaji ratiba kuna
umuhimu wa kuangalia mechi za kimataifa, kuwapa nafasi wawakilishi wan chi ambao
wanashiriki michuano ya kimataifa. Kwa hapa nyumbani tumebakiza timu moja tu
ambayo ni Yanga.
Ukiangalia ratiba ya Ligi Kuu Bara,
unaweza kudhani inaishambulia Yanga ili isifanye vizuri katika michuano ya
kimataifa. Lakini ninaamini haikuwa na nia mbaya, lengo ni kufanya mambo yaende
kwa utaratibu.
Pamoja na kutaka mambo yaende safi,
lakini inaonekana wanaopanga wamekuwa hawafikirii namna ambavyo wanaweza
kuzisaidia timu za nyumbani zinazoshiriki michuano ya kimataifa. Huenda Yanga
wanaona sahihi, lakini nina haki ya kukosoa au kuchangia ninapoona si sawa.
Yanga itashuka kuivaa Al Ahly ya Misri
kati ya Machi Mosi au Machi 2, hiyo itakuwa ni Jumamosi au Jumapili ijayo. Kumbuka
watakuwa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya wapinzani wao wakubwa baada ya
Simba na Azam FC, Prisons pia wana ushindani wa juu.
Mechi ya Yanga dhidi ya Prisons ni kati
ya big match katika soka hapa nyumbani. Kama Yanga itacheza Jumamosi dhidi ya
Al Ahly, maana yake itakuwa imepumzika mbili tu baada ya kucheza na Prisons halafu
itawavaa wababe hao wa Afrika, si kitu cha kawaida.
Bado itakuwa hivi, kama Yanga itacheza
Jumamosi, maana yake ndani ya siku nne, itakuwa imecheza big match mbili. Nafikiri
bado si sahihi kwa maana ya mwendo wa timu zetu, ninaamini Yanga wanaweza
kujitutumua, jambo ambalo ni nzuri lakini ratiba lazima ziwe na ufundi wa
kuzisaidia timu zinazoliwakilisha taifa katika michuano ya kimataifa.
Angalia Al Ahly mechi yao ya mwisho
ilikuwa ni jana dhidi ya Misr Lel Makasa na baada ya hapo watakuwa na siku tano
bila mechi na utaona timu waliyopangiwa ingawa watapumzika siku hiyo.
Hii inawapa funzo wataalamu wa TFF, kwamba baada ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting, Yanga ingepewa nafasi ijiandae.
Hii inawapa funzo wataalamu wa TFF, kwamba baada ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting, Yanga ingepewa nafasi ijiandae.
Kuaicha icheze tena katikati ya wiki,
bila kuangalia suala la majeruhi, uchovu na tena wanapokuwa na mechi ngumu au
kubwa dhidi ya timu kama Prisons, ni kuwaingiza Yanga kwenye dimbwi la hofu au
dalili za kutofanya vizuri.
Hapa inaonyesha namna ambavyo watalaamu
wa Shirikisho la Soka la Misri (Efa) wanavyojua umuhimu wa timu
inayoliwakilisha taifa lao katika michuano ya kimataifa. Hili hata wale wa TFF
wanapaswa kujifunza.
Wataalamu hao wa Efa wanaipa Al Ahly
siku moja ya kusafiri na si siku nzima, maana si zaidi ya saa 5 kutoka Cairo
hadi Dar. Lakini wameonyesha wanaelewa wanajua umuhimu na ugumu pia wa mechi
dhidi ya timu inayotoka kwenye taifa lingine. Kumbuka ni ligi ya mabingwa, wanaokutana
ni mabingwa wa nchi mbalimbali.
Lakini TFF walipaswa kujua Yanga inakutana na Al Ahly ambao ni mabingwa wa Afrika, au wangeweza kuweka tahadhari mapema, hapa lengo si ushabiki au kumfurahisha nani. Badala yake ni utaifa kwa kuwa tu Yanga wanaiwakilisha Tanzania, nchi yetu ambayo ndiyo kwetu.
Hivyo, TFF wanaweza kushiriki kuwasaidia Yanga kufanya vizuri, ratiba inayowapa nafasi ya kujiandaa vizuri ni sehemu ya kuonyesha utaifa. Pia hii isingefaa kwa Yanga tu, badala yake kila timu itakayopata nafasi ya kuliwakilisha taifa katika michuano ya kimataifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment