Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda kamati ya watu tisa kuratibu maadhimisho
ya miaka 50 tangu TFF ilipojiunga na Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa).
Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ni
Miss Tanzania mwaka 1999, Hoyce Temu.
TFF ilipata uanachama wa shirikisho
hilo la kimataifa Oktoba 8, 1964 ambapo itaadhimisha miaka hiyo 50 kwa kufanya
shughuli mbalimbali za mpira wa miguu.
Kamati hiyo itaongozwa na Mhariri
Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali, Gabriel Nderumaki wakati Katibu
atakuwa Lina Kessy ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Mwenyekiti
wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake (TWFA).
Wajumbe ni Ahmed Mgoyi, Hoyce Temu,
Teddy Mapunda, Ruge Mutahaba, Richard Kasesela, Boniface Wambura na Meneja
Biashara wa TFF anayetarajiwa kuajiriwa hivi karibuni.
Kamati itafanya kikao chake cha
kwanza Jumatatu (Machi 3 mwaka huu) kwenye hoteli ya Courtyard iliyopo Upanda
Seaview saa 7 mchana.
0 COMMENTS:
Post a Comment