Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) linaitakia kila la kheri yake kwenye mechi yake ya kwanza ya raundi ya 16
bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly kutoka Misri.
Mechi hiyo inachezwa kesho (Machi 1
mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia 10 kamili jioni. Timu hizo
zitarudiana Machi 9 mwaka huu jijini Cairo, Misri.
Maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika
ambapo kamishna Abbas Sendyowa kutoka Uganda na waamuzi wanne kutoka Burundi
tayari wapo nchini kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuvuta maelfu ya
washabiki.
Milango yote katika uwanja huo
itakuwa wazi, ukiwemo ule wa upande wa Uwanja wa Ndani (Indoor Stadium) wakati
Barabara ya Taifa (Taifa Road) itafungwa kuanzia chuo cha DUCE hadi msikitini
kuanzia saa 4 asubuhi.
Magari maalumu yenye sticker pekee
ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani. Vilevile washabiki wanakumbushwa kuwa
hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha au vifaa vyovyote vya chuma.
0 COMMENTS:
Post a Comment